0
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelakiwa kwa kishindo na wananchi wa Mwakata-Kahama waliopatwa na maafa wiki iliyopita.
Mara baada ya kuwasili Dk. Slaa amewasilisha mchango wa CHADEMA kwa Kamati ya Maafa kwa ajili ya waathirika hao. Mchango huo ni bundle 50 za mabati, BUNDLE ina mabati 16 ya gage 30 kwa gharama ya 12.5M,ni sawa na mabati 800. Ukijumlisha na milion10 alizotoa mh.freeman mbowe inakuwa milion 20.5
Akitoa pole kwa umati wa wananchi wa kijiji hicho Dr Slaa amewaambia chama chao cha Chadema ambacho ndicho kinaongoza serikali ya kijiji hicho kipo nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
Baadae mchana kiongozi huyo atakuwa na mkutano wa hadhara Isaka, Jimbo la Msalala.
Katibu Mkuu atapata fursa ya kutoa shukrani kwa wananchi wa Kanda ya Serengeti (zamani Ziwa Mashariki) kwa namna walivyoipatia heshima kubwa CHADEMA na kuonesha kuwa wana matumaini makubwa na chama hiki.
Kanda hii ndiyo iliyoongoza miongoni mwa kanda 8 za Tanganyika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kupata asilimia 48 ya kura za mitaa, vijiji na vitongoji vyote katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.

Post a Comment

 
Top