0

Uhusiano kati ya Rais Earnest Bai Koroma na makamu wake wa rais Sam suma sio mzuri
Makamo wa rais wa Sierra Leone, Samuel Sam Sumana, anasema kuwa anaomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.
Hayo yanafuatia ripoti kuwa wanajeshi wameizingira nyumba yake, na kuwanyang'anya silaha walinzi wake.
Juma lilopita, Bwana Sam Sumana alitolewa katika chama tawala, cha APC, akishutumiwa kuwa alichochea fujo,alikuwa na shahada za masomo za uongo, na kudanga-nya kuhusu dini yake.
Mwisho wa mwezi uliopita alijiweka karantini, baada ya mlinzi wake mmoja kufariki kwa sababu ya Ebola.
Alisema kuwa atajitenga na watu wengine kwa siku 21.

Post a Comment

 
Top