Refa allipepigwa marufuku
CAF pia inataka Tunisia kuomba msamaha kwa kutoa madai kwamba shirikisho hilo linapendelea mataifa kadhaa.
Tunisia pia imeagizwa kulipa faini ya uharibifu wa mlango pamoja na friji katika chumba cha kujiandaa katika uwanja wa Bata.
Refa
aliyesimamia mechi ya robo fainali kati ya Tunisia na waandalizi wa
kombe la Afrika Equitorial Guinea amepigwa marufuku ya miezi sita na
shirikisho la soka barani Afrika CAF baada ya kuwapatia Equitorila
Guinea penalti katika mazingira ya kutatanisha kabla ya timu hiyo
kushinda mechi hiyo 2-1..
Maafisa wa Tunisia walimvamia
Rajindraparsad Seechurn,baada ya mechi hiyo kukamilika na shirikisho lao
la soka limepigwa faini ya dola 50,000.CAF pia inataka Tunisia kuomba msamaha kwa kutoa madai kwamba shirikisho hilo linapendelea mataifa kadhaa.
Tunisia pia imeagizwa kulipa faini ya uharibifu wa mlango pamoja na friji katika chumba cha kujiandaa katika uwanja wa Bata.

Post a Comment