0


Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea leo, Timu ya Yanga SC ilikuwa kwenye dimba la Mkwakwani Tanga ambapo wanajangwani hao walikuwa wakichuana na wenyeji wa Tanga, Coastal Union mechi ambayo imeisha muda mfupi uliopita.
Katika mechi hiyo dakika 90 zilikamilika pamoja na zile  tatu za nyongeza kwa Yanga kushinda goli 1-0 dhidi ya Coastal Union.
 Timu hizo zilishambuliana kwa zamu na hakukuwa na burudani, zaidi ya ‘butua butua’, kushindana nguvu na kasi, kutokana na timu zote kuhofia kucheza ‘kandanda ya kitabuni’ kwa sababu ya hali mbaya ya Uwanja wa Mkwakwani.
Kipindi cha pili, Yanga SC walianza kucheza kwa kujihami kulinda bao lao, huku wakifanya mashambulizi machache ya kushitukiza.
Coastal Union ilikaribia kusawazisha bao dakika ya 82 baada ya Godfrey Wambura kumpa pasi nzuri, Hussein Sued, ambaye licha ya mabeki wa Yanga kumuacha wakidhani ameotea, lakini akapiga nje akiwa ndani ya sita.

Kwa ujumla mchezo ulikuwa wa ‘kindava ndava’ na hakukuwa na burudani yoyote- na sifa ziwaendee marefa wa mchezo wa leo kwa kuumudu vyema.
Kipindi cha kwanza mashabiki wa Coastal waliwavurumushia mvua ya mawe mashabiki wa Yanga, hadi Polisi wakaenda kuwasaidia.
Kikosi cha Coastal Union kilikuwa; Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Sabri Rashid, Abdallah Mfuko, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Said Mtindi dk60, Godfrey Wambura, Hussein Sued, Rama Salim na Itubu Imbem. 
Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Said Juma ‘Kizota’, Kpah Sherman, Amisi Tambwe/Danny Mrwanda dk83 na Andrey Coutinho/Hussein Javu dk65.

Post a Comment

 
Top