Rais wa Zimbabwe mh.Robert Mugabe
EU yalegeza vikwazo walivyomuwekea mugabe
Umoja wa Ulaya umesema kuwa, umemuondolea Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe marufuku ya kusafiri, katika kipindi hiki akiwa Mwenyekiti mpya wa kiduru wa Umoja wa Afrika. Catherine Ray, msemaji wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa, marufuku hiyo itaondolewa wakati Mugabe atakapokuwa akifanya safari zake za nje chini ya mwavuli wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Umoja wa Ulaya uliiwekeza vikwazo Zimbabwe mwaka 2002 kufuatia kukiukwa taratibu za uchaguzi nchini humo na hivyo kupiga marufuku safari za nje ya nchi na kuzuia mali za makumi ya maafisa na wawakilishi wa kibiashara wa Zimbabwe. Hii ni katika hali ambayo, marufuku na vikwazo hivyo vimekuwa vikiondolewa awamu kwa awamu katika miaka kadhaa ya hivi karibuni ili kuhamasisha kufanyika mageuzi nchini Zimbabwe. Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umesema Jumanne hii kuwa, Rais wa Zimbabwe huwenda akaruhusiwa kushiriki kwenye mikutano ya ngazi ya juu ya umoja huo, akiwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, licha ya marufuku ya muda mrefu ya kusafiri iliyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa Rais huyo wa Zimbabwe.

Post a Comment