PICHA KUTOKA MAKITABA
Mwaandishi wetu Liwale….
Wananchi wa
kata ya Kipule kijiji cha Makinda wilaya Liwale
mkoani Lindi wamemtimua mbunge wa viti maalum,zainabu Kawawa
kwa madai kufanya mkutano wa kutangaza nia ya kuomba
ubunge katika jimbo hilo kabla ya muda
wa kufanya hivyo haujafika.
Tukio hilo limetokea juzi(alhamisi) majira ya saa nane mchana baada ya mbunge huyo kufika kijijini
hapo kwa lengo la kukutana na mwenyekiti
wa kijiji Salum Kachwele ili kumtaka
aitishe mkutano wa wajumbe wa
serikali ya kijiji na baadhi ya wananchi hasa wazee maarufu ikiwa ni
kuwashaawishi ili wamwuunge mkono katika harakati zake za kuwania ubunge wa jimbo
hilo.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya
kijiji hicho Salum Kachwele alisema mbunge huyo alifika kijiji hapo akiwa na
mpambe wake Mkopora Mkopara na kumuomba awaite wajumbe wa serikali ya kijiji
pamoja na wazee maarufu ili azungumze nao jambo ambalo alidai
hakulikubali kwani kabla ya harakati hizo za ubunge Kawawa hajawahi kufanya
kikao chochote wala kutembelea katika kijiji hicho.
Kachwela alisema
kabla zoezi la kukutana na wanachi hao
halijafanikiwa lilikuja kundi
kubwa la wananchi likiongozwa na vijana wakizomea wakiwa na mawe na
magongo waliotokea kwenye mkutano wa chama cha wananchi cuf waliokuwa kwenye
mkutano wakuwashukuru wananchi kwa kukichangua cha hicho kwenye uchagunzi wa
serikali uliopita na kumtaka mbunge huyo
kuondoka katika eneo mara moja.
Kwa upande
wake mbunge Zainabu kawawa alikiri
kutembelea kijiji hapo ila alikataa kufanya kikao na wananchi hao na kutokea tukio la kufukuzwa na kueleza kuwa
yeye alikwenda kufanya ziara ya kikazi ya kuwatembelea wapiga kura kuhamasisha
maendeleo.
‘Ndugu yangu hayo maneno sio kweli mimi nilikwenda
kijiji hapo kufanya kazi za kibunge sio kufanya kampeni kama ilivyoelezwa na
hao watu wasionitakia mema’ukweli ni kwamba
mti wenye matunda matamu ndiyo unapigwa mawe alisema Kawawa.SAUTI YA KUSINI
Post a Comment