0
Chadema wafanya mkutano mkubwa wa hazara wilayani liwale uliohutubiwa na katibu mwenezi Bavicha Taifa bwana Edward Simbei ulifanyika katika viwanja vya Nanjinji  jana.


                                    viongozi wa  chadema

wanachama na wakeleketwa walioudhulia kwenye mkutano ulifanyika katika viwanja vya Nanjinji

Ziara ya katibu mwenezi wa Bavicha Taifa ni kuimarisha chama hicho,katika mkutano huo chama cha chadema kimesema kitashughulikia suala la ucheleweshaji wa ugawaji wa viwanja kwa wananchi waliochangia gharama zote za upimaji iliyopendekezwa mwaka 2009 katika Halmashauri ya Liwale.Uchelewechwaji wa ugawaji viwanja umetokea mara baada ya halmashauri kuweka bei mpya na wananchi waliochangia kugomea bei hiyo.

Chama kimesema kitatoa nots za siku 30 kwa halmshauri ya liwale ili iweze kuwagawia wananchini waliokamilisha uchangiaji wa viwanja hivyo kama halmashauri itashindwa kutekeleza chama kupitia wakili na mwanasheria wao wa chama  halmashauri itaburuzwa mahakani.Pia wamewataka wananchi ambao waliochangia viwanja hiyo ambavyo mpaka sasa hawajapata leo waende na barua zao za maombi na risiti zote za malipo katika ofisi ya chadema waweze kujiorodheza na kuweka sahihi zao.

Halmashauri ya Liwale ilitoa tangazo lake la bei mpya ya viwanja hiyo mara baada ya viwanja kupimwa huku wananchi walioomba walichangishwa kwa bei ya mwaka 2009. Tangazo likuwa na  kumb na LW/DC/D.10/49 la Tarehe 30/11/2014 baada ya kamati ya ugawaji viwanja ya wilaya iliyoketi na kuazimia mapendekezo ya upimaji kilichofanyika tarehe 28/10/2014.Tangazo hilo lilieleza jinsi ya ongezeko la bei kwa wale waliochangia awali walitakiwa;-

WOTE WALIOPATA VIWANJA WANATAKIWA KUZINGTIA YAFUATAYO
.Kufika ofisi ya Ardhi (W) Liwale na kuchagua kiwanja kulingana na matakwa yake (kuanzia tarehe 4/11/2014 hadi tarehe 5/11/2014 na tarehe 10/11/2014 na kuendelea katika ofisi ya Ardhi ya wilaya ya Liwale.Aidha watatakiwa kuwasilisha fomu halisi ya maombi ya kiwanja (Land form no.19) aliyopewa wakati wa kuchangia na nakala ya risiti ya malipo aliyopewa wakati  uchangiaji.

Kufanya malipo ya kiwanja kulingana na gharama ambazo zitakuwa zimeongezeka.
Mwananchi atapewa fomu inayoonyesha gharama ya kiwanja (voucher)alichochagua na atatakiwa kwenda bank kulipia kiasi ambacho kimeongezeka katika gharama alizochangia upimaji hapo awali.

NB.Bei ya viwanja hivi zinatofautiana na kulingana na ukubwa wa kiwanja kwa mita za mraba na matumizi ya kiwanja husika,bei hizi zimetokana na gharama halisi zilizotumika katika upimaji,gharama za ulipaji wa fidia ya mashamba ya wananchi yaliyotakiwa kwa ajili ya upimaji wa viwanja.

Bei mpya ya viwanja kwa sasa                    Bei ya kila mita ya mraba  tsh.  
a juu,kati na chini)

 Makazi pekee                                                 600
Makazi na biashara                                          750
Huduma za jamii                                               600
Ibada/kuabudu                                                 600
Viwanda vidogo vidogo                                    900
Makazi maalumu                                              900

Post a Comment

 
Top