Mwaandishi wetu Liwale
MKAZI wa kijiji cha
Kibutuka,wilaya ya Liwale,mkoani Lindi, Mustafa Kinyuwile (40) amekufa papo
hapo,baada ya kushambuliwa na tembo,alipokuwa na wenzake wakiwinda wanyama
katika msitu wa hifadhi ya maliasili wa Serou.
Kwa mujibu wa kamanda
wa Polisi mkoani hapa,Renatha Mzinga,akizungumza ba waandishi wa habari alisema
kuwa Kinyuwile alikutwa na mkasa huo,Decemba 31/2014,saa 8:15 mchana ambapo
waliingia kwenye hifadhi hiyo bila ya kuwa na kibari kinachowaruhusu kufanya
hivyo kutoka mamlaka husika.
.
Mzinga alisema siku
hiyo,Kinyuwile akiwa na wenzake wawili, aliowataja kuwa ni,Chande Mtabiaga na
Mateso,walikuwa kwenye msitu huo wakifanya shughuli za uwindaji kwenye msitu
huo wa Hifadhi,ndipo tembo huyo aliyekuwa katika himaya yake alianza kuwafukuza
na kufanikiwa kumpata mmoja wao.
Alibainisha kuwa
baada ya Kinyuwile kuuawa na tembo huyo, Mtabiaga na Mateso waliuchukuwa
mwili wa mwenzao kisha kuutelekeza eneo la kijiji cha Kilangala,badala ya
nyumbani kwake na wao kuondoka kusikojulikana.
“Huyu mwili wa huyu
marehemu ulikutwa umetupwa eneo la kijiji cha Kilangala,huku umenyofolewa jicho
la kulia na mbavu zake zikiwa zimepondwa pondwa”Alisema Kamanda Mzinga.
Kamanda Mzinga
alisema katika ufuatiliaji wao wa awali jeshi la polisi limebaini wawindaji
hao,walikuwa wakifadhiriwa na mfanyabiashara wa vifaa vya pikipiki aliyemtaja
kuwa ni,Kasimu Mtabiaga (51) ambaye ni ndugu watu aliokuwa akishirikiana na
marehemu Kinyuwile katika shughuli zao za uwindaji.
Amesema tayari
wanamshikilia mfanyabiashara huyo kwa mahojiano zaidi,huku akisubiri taratibu
zingine za kisheria.
“Kwa sasa jeshimletu
linamshikilia kaka yake marehemu kwa mahojiano zaidi,ikiwa ni
pamoja na kutuwezesha kuwapata hawa wenzake,ili sheria iweze kuchukuwa mkondo
wake”Alisema Mzinga.
Kamanda huyo wa Polisi mkoani Lindi,Renatha Mzinga amezidi kutoa wito
kwa kuwataka wananchi kuacha tabia ya kuwinda bila ya kufuata utaratibu
uliowekwa na Serikali.KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Post a Comment