PICHA KWA HISANI YA FAHARI YA KUSINI
Ujenzi wa barabara ya Kilometa
60 kati Ndundu Rufiji hadi Somanga wilayani Kilwa kwa kiwango cha Lami kwa kutumia fedha za mapato ya ndani
zilisababisha nchi ya Kuwait kurejea tena na kushirikiana na serikali kujenga
barabara hiyo baada ya awali kutotoa Fedha licha ahadi
Hayo yameelezwa na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mhandisi Mussa
Iyombe wakati wa Ukaguzi wa barabara
hiyo uliofanyika kijijini Somanga wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Mhandisi Lyombe alisema nchi ya Kuwait ilisita kuendelea
kufadhili ujenzi barabara hiyo yenye urefu wa kimometa 60,serikali iliendelea
na ujenzi kwa kutumia fedha za ndani Ambapo awali ilikadiriwa ujenzi huo ungegharimu shilingi bilioni 58 Ha ta hivyo
kutokana na ujenzi huo kuchelewa kukamilika, gharama ilipanda na kufikia
shilingi bilioni 66 hadi kukamilika.
Pamoja na kuruhusu kutumika kwa barabara hiyo baada ya
kuunganishwa kati ya kijiji cha Marendego na Somanga Iyombe aliwaasa watumiaji
wa barabara hiyo ikiwamo madereva na
watembea kwa miguu kuitunza barabara hiyo ambapo Kwa upande wao baadhi ya madereva licha ya
kuishukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo huku wengine
wakiomba kutengenezwa kwa barabara zingine zinazounganisha Wilaya hata kwa
kiwango cha changarawe ikiwamo barabara ya Ruangwa hadi Lindi,Nachingwea hadi
Nanganga na Masasi hadi Nachingwea kuanganisha na Wilaya ya Liwale
Awali Meneja wa wakala wa Barabara(Tanroads) mkoa wa Lindi Mhandisi Issack Mwanawima alieleza furaha yake baada ya kukamilika kwa barabara hiyo ya km 60 iliyojengwa Kwa zaidi ya Miaka 5 Toka ujenzi Uanze. SOMA HAPA
Post a Comment