Akizungumza
na vyombo vya habari katika eneo la tukio naibu waziri nishati na
madini mheshimiwa CHARLES KITWANGA amesema tukio hilo limetokana na mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za malawi na msubiji na hivyo
kuleta madhara upande wa tanzania.
Katika
kukabiliana na hilo naibu waziri amelazimika kuitisha kikao cha dharura
cha kamati ya ulinzi na usalama na kuona njia rahisi ni kutumia jeshi
la majini na nchi kavu ili kusaidia kuzuia sehemu ya kiwanda iliyobaki
isimezwe na maji.
Huku
muhandisi mkuu wa kiwanda hicho cha M and P PETER JOHN akisema endapo
ardhi hiyo itaendelea kumegwa wakati wowote watasitisha kazi ili
kunusuru maisha ya watu na mali zinazohamishika.
Mbali na
kiwanda hicho pia bomba kuu la gesi linalotoka baharini na kuisafirisha
gesi katika viwanda vya mtwara na lindi na hatimaye dar kinyerezi kwa
ajili ya kufua umeme wa gredi ya taifa nalo liko hatarini kuadhirika
kwani bahari imebakiza mita sita kufikia eneo la nchi kavu lilipo bomba
hilo.
Dhoruba
hiyo imetokea usiku wa tarehe 13 kuamkia tarehe 14 ambapo kipande cha
ardhi chenye ukubwa wa mita miamoja na sita kiliweza kumezwa na maji ya
bahari kwa muda wa masaa matatu.
Post a Comment