wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Ruangwa wakiwa kwenye kikao cha bajeti
Mwandishi wetu Ruangwa
BARAZA la madiwani Halmashauri ya Wilaya Ruangwa Mkoani Lindi limepitisha bajeti ya zaidi ya sh bilioni 20 zitakazokusanywa na kuelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016.
Kati ya kiasi hicho cha fedha,sh bilioni 1.627 zinatarajiwa
kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani ambapo
ruzuku kutoka serikali kuu na misaada kutoka kwa wafadhili ikitarajiwa kuwa ni
zaidi ya sh bilioni 4.8
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa maendeleo na
bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mwaka wa fedha mwaka 2015/2016
katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ruben Mfune alisema makadilio ya bajeti kwa
mwaka wa fedha wa 2015/2016 ni sh bilioni 20.361
Alisema makadilio hayo yamepanda kutoka sh bilioni 15.279 kwa
mwaka wa fedha wa 2014/2015 ingawa hadi kufikia Novemba 2014,Halamashauri hiyo
ilifanikiwa kukusanya jumla sh bilioni 5.657 kutokjana na vyanzo vya ndani sawa
na asilimia 34 ya makadilio yake.
Kwa mujibu wa mfune Halmashauri inatarajia kutumia bilioni
4.885 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia vyanzo
mapato kama vile ruzuku kutoka serikali kuu,vyanzo vya ndani pamoja na fedha
kutoka kwenye programu za Elimu
Sekondari (SEDP),Maji na Usafi (NWSSP) pamoja na Mfuko wa Barabara.
Alisema licha ya kupitisha makisio ya bajeti ya mwaka wa
fedha wa 2015/2016 Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo
huathiri utekelezaji wa malengo wa
utekelezaji yanayowekwa kama vile kucheleweshwa kwa fedha za ruzuku kutoka
serikali kuu, pamoja kutofikiwa kwa malengo ya
ukusanyaji mapato kwenye baadhi ya vyanzo vya Halmashauri.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ruangwa mkoani Lindi Ruben Mfune
akifafanua jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha bajeti
kilichofanyika hivi karibu kushoto kwake ni mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Isa Libaba na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Post a Comment