0


 
 Mwaandishi wetu Lindi
kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata mzinga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari 

SERIKALI Mkoani Lindi imetaka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  kubomoa vibanda vyote vilivyojengwa nje ya utaratuibu mara moja.
Agizo hilo lilitolewa jana na mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza wakatinalipokuwa akizungunza kwenye baraza maalumu la Madiwani wa Manispaa hiyo,alisema kuwa ni muhimu vibanda hivyo kubomolewa mara moja na watendaji wa mamlaka hiyo.
Natoa agizo hilo mara moja litekelezwe  kwani litasababisha kuleta vurumai kwa ujenzi holela,na hata kama sisiviongozi tuna vibanda vyetu,alisema Mahiza.
Alisema maofisa mipango miji,Mkurugenzi hakakikisheni kazi hiyo inafanyika kwa wakati unaotakiwa si tena kuleta kesho keshokutwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira  Asha Kigoleche alisema kuwa tatizo lipo katika baraza la Madiwani.
Alisema baadhi ya viongozi hususani haswa Madiwani na Mbunge mmoja wana vibanda vyao vilivyojengwa nje ya utaratibu ,lakini mpaka sasa havijabomolewa.
Alisema watendaji nao walishapewa taarifa nao wanasita kwani kuna kiongozi naye ni Mbunge naye alikiuka taratibu hizo za ujenzi.
Mwenyekiti huyo alisema hivi karibuni vilibomolewa baadhi ya vibanda vya madiwani vipatavyo saba.
Alisema kwa hiyo kutokana na ubomoaji huo sheria ni msumeno lazima nao wabomolewe.

Post a Comment

 
Top