mwenyekiti
wa kikao cha barabara mkuu wa mkoa wa Lindi Mwamtumu Mahiza akifungua
kikao hicho kwa kuwataka wajumbe kuwa wasikivu na kuchangaia kwa
umakini.
mwaandishi wetu Lindi……
Wakala
wa barabara mkoani Lindi wameombwa kuziangalia barabara zao za
zilizoko wilayani Ruangwa ili kunusuru maisha ya watu na mali zao.
Ombi
hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Ruangwa Agnes Hokororo kwenye kikao
cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa
Lindi
Hokororo
alisema barabara ya Nanganga kwenda wilayani Ruangwa ipo katika hali
mbaya na madaraja yana matatizo na baadhi ya maeneo katika barabara
hiyo yamegeuka kuwa njia ya maji na makazi ya watu yapo mashakani.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Isa Libaba alisema barabara
zinazohudumiwa na Tanroad zinahitaji matengenezo , hivyo ni vyema
wataalamu na watendaji wa mamlaka hiyo wakatembelea barabara hizo
kujionea hali halisi ya uharibifu unaofanywa na mvua za masika
zinazoendelea kunyesha.
Kwa
upande wake meneja wa Tanroad mkoa wa Lindi injinia Isack Mwanawimba
alisema kuwa ofisi yake inatambua kuwepo kwa matatizo
madogomdogo wakati huu wa masika na ufanya marekebisho ya haraka
kwenye maeneo ya barabara yanayoaribiwa na mvua ili kuwafanya watu
waendelee kutumia
Post a Comment