0


  Maandishi siku zote hubaki na maana kama watu watayazingatia maana yake.Karibu ubarizi


         
. Liwale ina Mkukuyumbu walikouawa askofu na masista

. Pia kuna Boma la Mjerumani linalohitaji kurekebishwa

. Lipo pia Kaburi la Ndapata linalofagiliwa kwa heshima





UTAFITI
Mwaka 2009

UKIFIKA katika mji wa Liwale na ukataka kuulizia masuala ya historia na utamaduni wa eneo hilo hutakuwa na hamu ya kuondoka kwa msimulizi wako kutokana na eneo hilo kuwa na moja ya matukio makubwa ya kihistoria katika kuingia kwa wamisionari na pia vita ya majimaji ambayo iliuma sana katika maeneo ya ukanda wa Pwani kuanzia mwaka 1905hadi 1907 mambo yalipokuwa shwari kabisa.

Wamisionari walikwepa eneo hili kwa miaka mingi kutokana na jinsi watu wake wa kwanza walivyofanyiwa vibaya katika msuguano mkubwa wa kutaka kumuondoa mkoloni nchinina siasa zake zilizokuwa kero kwa wananchi hasa kuhusiana na kodi na pia ulimaji wa pamba.

Kilomita 40 kutoka liwale katika njia inayowenda Dar es salaam kupitia Njinjo eneo la Mkukuyumbu ndiko kuliko na alama ya tishio kwa wamisionari,mahali alipouawa askofu Spiss na masista wake watatu.hapa ndipo pana kaburi la Askofu huyo na masisita hao. Spiss alikuwa Askofu wa kikatoliki wa dare s salaam na msafara wake huo mdogo ulikuwa na jumla ya watu watano.

Hadithi ya kuuawa kwa msafara huo wa wamisionari ni ndefu kidogo kwani ina uhusiano mkubwa na vita ya Majimaji iliyoanzishwa na Kinjeketile kwa lengo la kuondoa utawala wa Kikoloni kwa kukutanisha fikira za watu utamaduni na imani zao.

Watu waliaminishwa kwamba dawa waliyopewa itabadilisha risasi za mzungu kuwa maji na kwa kuwa makabila ya pwani ambayo yana utamaduni unaofanana walikuwa na mizimu ambayo inaheshimiana,kasi ya vita iliuma na ama hakika ilikuwa mbaya zaidi inavyofikiriwa.

Ni vyema kwa sababu za kihistoria tu kukumbusha kwamba vita ya maji maji haikuanzwa na Wangindo bali na mganga mmoja kwa jina Kinjikitile Ngwale ambaye alidai kumilikiwa na mzimu wa Hongo ambao ulisema kwamba wakati umefika kwa wananchi wa Afriika Mashariki kuwachomoa wajerumani na siasa zao za kushinikiza kilimo cha pamba. Ngwale ambaye baadaye alijiita Bokero aliwaambia wafuasi wake kwamba wasiogope risasi za wajerumani kwani zitageuka kuwa maji baada ya kunywa na kujiosha kwa dawayenye mafuta ya mbarika yaliyochanganywa na mbegu za mtama.

Wakiwa wamejivika mabua ya mtama katika sura zao shughuli ilianzia Samanga Julai 31,1905 ambapo wamatumbi walivamia maeneo kadhaa ya kiserilkali na kuharibu mashamba ya pamba. Mambo yalitulia Agosti 1907 lakini baada ya chakaza isiyo na ustaarabu ya Wajerumani.

Ingawa takwimu zinaonyesha kwamba askari wa kizungu 15 na 389 wa Kiafrika waliuawa katika patashika hiyo wakati wapigania uhuru (waasi) kati ya 200,000 na 300,000 walikufa kwa risasi za Mjerumani na pia kwa njaa, kashkashi ya kuuawa kwa wamisionari hao huko Liwale pamoja na kuchomwa moto kwa makao makuu huko peramiho katika miaka hiyo ni moja ya matukio la kihistoria ambayo yanaipa Liwale nafasi ya masimulizi ya kilichotokea katika vita hiyo.

Pia inatoa nafasi ya kueleza wazi kwamba huenda tukio hilo ndilo lililofanya eneo la Liwale hasa maeneo ya Ungindo kubaki na dini ya kiislamu kwa muda mwingi zaidi.

Baada ya kufanya mauaji hayo ya wamisionari,Mapanda alifanikiwa kuwatega wanajeshi wa Kijerumani na kuwalazimisha kujinasua katika mtego na kuondoka eneo hilo la Ungindo kwa muda. Kwa miezi mitatu Mapanda alitawala huku akiitisha baraza la utawala katika eneo la Kingwichiro.

Wakati naingia Liwale wiki iliyopita,Wakristo wa Assemblies of God (kama sikukosea-lazima nikiri kwamba haya makanisa ya kipentekoste wakati mwingine anuani zao zinanichanganya) walikuwa wanazindua kitabu kimoja cha Biblia kwa lugha ya Kingindo na walimwalika mkuu wa wilaya Paul Chiwile kufanyakazi hiyo.

Wainjilisti hawa wapya walikuwa wanataka kupeleka Biblia kwa wananchi wa hapa kwa lugha yao wenyewe. Wamisionari hao wapya wamesema kwamba wamepania kuhakikisha kwamba Biblia nzima wanaitafisiri Kingindo kwa manufaa ya wananchi wa Kingindo.

Ukiachia simulizi hiyo ya kuuawa kwa wamisionari hao wa kwanza wa dhehebu la Kikatoliki la Kibenedikti kati ya Agosti 13 na 14 (imeandikwa mahali ni Agosti 14), mauaji yaliyotanguliwa na kushambuliwa kwa Boma la Mjerumani Agosti 13 na Wangindo wakiongozwa na Abdallah Mapanda wa Kingwichiro na kuliteketeza kwa mishale inayowaka lipo Boma la Kijerumani mwendo kidogo kutoka kitovu cha mji, eneo ambalo ulikuwapo mji wa awali.

Kaimu ofisa utamaduni wa wilaya ya Liwale ambaye ndiye alikuwa mwongozi wangu katika kusaka historia na matukio ya kukumbukwa wilaya ya Liwale Shaibu Ulochi alisema kwamba kama wilaya yake ingelipatiwa njenzo za kutosha wangelijitahidi sana kuhakikisha historia ya aneo hilo inahifadhiwa inavyostahili kwa vizazi vijavyo.

Amesema pamoja na maelekezo ya wizara ya utamaduni lakini hakuna uwezeshaji si kutoka serikali kuu au halmashauri ambao unapangwa kuendeshea shughuli hizo za kuhifadhi sanaa , utamaduni, mila na hata historia ya eneo hilo.

Amesema Boma la wajerumani lililojengwa mwaka 1905 hapo Liwale ukiachia lile ambalo lilichakazwa na moto kutokana na paa lake kuwa la majani linaendeleas kupoteza uwzo wake na ingawa bado linatumika linastahili matengenezo makubwa ili kuwa baadaye moja ya kielelezo cha kuwapo kwa Wajerumani katika eneo hilo.

Liwale ingawa inakumbukwa sana kwa vita ya majimaji na jinsi wananhchi walivyoshiriki katika jaribio la kumuondoa mkoloni pia kuna maeneo ya matambiko ya Kingindo na pia lipo kaburi na Mwanamama mmoja ambaye alikufa katika miaka ya karibuni ambapo wananchi mara nyingi hufika kulisafisha na kuomba baraka. Kaburi hilo lipo Ndapata.

Kwa mujibu wa Shaibu mama huyo hakuwa mganga wa kienyeji lakini alikuwa na karama nyingi za kuzuia mabalaa na pia kuombea neema.

“Mimi ni Mngindo naelewa hili la Uganga wala hakuwa mganga kwani mganga anahitaji zana zake; na wala hakuwa anafanyakazi za uganga huyu ni kama vile ulivyouliza ni aina ya sharifu,alikuwa na karama za kama za mwanaume na hata viongozi wengi wakubwa walikuwa wanamtembelea kabla hajafa mwaka 1975” alisema Shaibu.

Alisema mama huyo alikuwa na nuwezo wa kuondoa janga la simba wanaposhambulia pia kuita mvua inapopotea au inapokuwa zaidi na kuifanya iwe ya kawaida.

Injafaa ikumkbukwe pia hapa kwamba Liwale ipo katika eneo la hifadhi ambapo Simba wakati mwingine huvamia makazi ya watu na watu walipoenda kumlilia mama huyu awasaidie samba hao walirejea porini wasionekane tena.

Shaibu aliwataka wakubwa wengi tu waliokuwa wakitembelea Liwale walifika kumjulia hali mama huyo ambaye anasema alikuwa ni swala tano.Sedhemu kubwa ya Ungindo ambayo nni Liwale ina waumini wa Kiislamu.

Kipaji cha pekee cha mwanamama huyo kinafanya bado hata umautini awavutie watu kwenda kulisafisha ziara lake kila wanapofika Liwale au kurejea Liwale. Na hata watu wengine wa Liwale kutoka maeneo yao hufika Ndapata kuzuru kaburi hilo na kulifanyia usafi.

Alisema hali ilivyo sasa kama maeneo kadhaa yasipohifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo ipo hatari kubwa kwa vizazi vijavyo kukosa simulizi halisi la nini kilikuwapo au kutokea na kutegemea zaidi watu wa utafiti kutoka nje.

“ sehemu kubwa ya mambo haya ya kihistoria yapo midomoni mwa watu na kama tusipofanya juhudi za sasa kutafuta na kuhifadhi hatuwezi kuwa nayo baadaye” alisema Shaibu ambaye bado anadhani serikali ina wajibu mkubwa wa kuainisha nvitu na kuanzisha makumbusho kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo wakati dunia ikiwa inabadilkika zaidi.

Alisema hifadhi za kihistoria sita itasaidia kuelewa mambo zamani yalikuwaje bali pia ni kwa namna gani wananchi wa hapo zamani walivyofanikisha maisha.

Amesema mathalani hali ya boma ya mjerumani kwa sasa si nzuri lakini kama likitengenezwa litabi vyema kwa miaka kadhaa ijayo ikiwa ni mojaya alama ya kuwapo kwa watawala wa kigeni nchini.

Pia masimulizi kama majimaji ilivyopiganwa na namna imani ya mizimu ilivyochangia vita hiyo,tutalazikika kununua habari hizi kutoka kwa wengine ambao wataandika kwa jinsi wnaavyoona inawasaidia wao na kuuacha ule ukweli kuwa vita hii ilikuwa ya ukombozi.

Akizungumzia mambo mengine yanayosimamiwa na mofisi yake amesema sanaa ya maigizo,maonyesho imeanza kufufuliwa katika wilaya hiyo kwa kuwa inaonyesha kusaidia sana watu kuelimika.

Aidha amesema kwamba kila kijiji kina kikundi cha sanaa ingawa walivyosajili vikubwa ni viwili vya Uwaki na Kauli mbiu ambavyo vyote vinashiriki katika sanaa za maonyesho.

Akizungumzia utajiri wa mila alisema kwamba Liwale ina mila nyingi nzuri lakini pia nzipo ambazo zinaleta shida kidogo kama utamaduni wa kuhama katika kilimo, uchomaji moto mapori, namna ya kutahiri watoto na pia shauri zima la kurithi wajane.

Amesema kuhama kutafuta mahali pa kilimo , hali ambayo mimejenga miaka mingi katika maisha ya wananchi wa wilaya Liwale inaharibu mazingira na pia kunyima fursa watoto kwenda kutafuta elimu.Amesema wananchi wa Liwale hukata misitu daima na kulima na akiona ardhi imechoka huondoka kwenda kutafuta pori jingine.

Kimsingi bado ni tatizo la uharibifu wa mazingira kwa tabia hiyo na pia kitendo hicho huinyima fursa serikali kusaidia maendeleo katika sekta ya elimu na afya.

“watu wanaohamahama huwa shida sana kufikiwa na huduma za serikali” alisema Shaibu.

Diwani wa viti maalum wa CCM liwale B Anna Simba alisema moja ya vcita kubwa ambayo wnaayo ni kushawishi wananchi kuondokana na tabia za kulima kwa kuhamahama kwa kusisitiza matumizi ya pembejeo kama mbolea na ulimaji wa kisasa zaidi katika kutoa mazao mengi.

Alisema baraza la madiwani kwa kushirikiana na halmashauri wamekuwa wakiendesha kampeni kubwa ya kutaka wananchi watulie maeneo husika ili serikali iweze kuwahudumia.

Tabia nyingine ambayo ilielezwa ni uchomaji moto kwa lengo la kujua umri mtu atakaoweza kuishi. Inadaiwa kwamba moto ukilamba sehemu kubwa yam situ basi wewe utaishi maisha marefu, dhana hii inaangamiza misitu na kufanya idara ya utamaduni kuanza kampeni ikisaidiana na idara nyingine kuipiga vita mila him potofu kwa kutumia mikutano na pia vipeperushi.

Pia tabia ya kupeleka jandoni watoto zaidi ya 10 na kuwatahiri kwa kutumia kisu kimoja, pia inaleta shida ya kuambukizana na magonjwa nayo inastahili kupigwa vita.

Upigaji vita wa mila hii, anasema Shaibu si wa kuitaka watu waache bali watumie njia za kisasa zaidi katika kufanikisha suna ana hivyo kuondoa uwezekano wa kuambukizana magonjwa.

Post a Comment

 
Top