Madaktari
katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini Kenya,Kenyatta,
wamefanikiwa kuondoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa mtoto
Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.
Mamake
Satrine alikuwa amempakata mtoto wake ili kumlinda kutokana na magaidi
waliovamia kanisa walimokuwa wiki moja iliyopita katika mtaa wa Likoni
mjini Mombasa.
Lakini
walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua
mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo wake.
Satrine alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa kutokana na ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli
ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na madaktari
watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa kitengo cha
upasuaji wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo.
SOURCE:BBC
Post a Comment