Umoja wa Mataifa unasema hali ya
usalama katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati imeendelea
kuzorota, huku taharuki ikiendelea kutanda kati ya walinda amani na
wapiganaji wa kikristo Anti -Balaka.
Taarifa zinasema kwamba zaidi ya watu 20
waliuawa na 100 kujeruhiwa hapo Jumamosi wakati wanajeshi wa Chad
walipowafyatulia risasi wakaazi wengi ambao ni WakristoShirika la Umoja huo la kuwahudumia wakimbizi, linasema kuwa maisha ya maelfu ya waisilamu yamo hatarini kwani wengi wanakabiliwa na tisho la kuuawa na wakristo
Shirika hilo linajaribu kuwahamisha wakimbizi 19,000 waisilamu wanaoishi katika vitongoji vinavyozingira mji mkuu Bangui.
Shirika shirika hilo limesema kuwa karibu watu elfu kumi na sita wameachwa bila makao katika siku kumi zilizopita.
Zaidi ya watu 20 kati ya waliofariki waliuawa na wanajeshi wa Chad waliowafyatulia risasi Jumamosi katika mtaa wenye wakristo wengi.
Kwa mujibu wa Umoja huo, wapiganaji wa kikristo wamezidisha mashambulizi dhidi ya waisilamu na walinda amani wa Muungano wa Afrika.
Vurugu zilianza mwezi Machi, baada ya waasi wa Seleka kumwondoa mamlakani Rais mwezi Machi mwaka 2013
Licha ya kupelekwa kwa wanajeshi 6,000 wa muungano wa Afrika pamoja na wanajeshi wengine 2,000 wa Ufaransa, vita vimekuwa vikikithiri.bbcswahili
Post a Comment