Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu
Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema mizoga ya tembo 39 ilionekana
ndani na nje ya Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba nchini katika kipindi
cha kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
jijini hapa jana, Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa wizara hiyo,
Ibrahim Musa, alisema katika kipindi hicho meno mazima 171 na vipande 22
vya meno ya tembo ghafi, vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa
yenye jumla ya kilo 662.62 yalikamatwa.
Pia alisema katika kipindi hicho jumla ya kilo 1,111 za nyamapori za wanyama mbalimbali zilikamatwa.
Alisema bunduki moja ya rashasha, rifle tatu, shotgun mbili, gobori tano na jumla ya risasi saba za aina mbalimbali zilikamatwa.
Alitaja mali na vifaa vingine vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na magari matano yaliyohusika katika ujangili hasa wa meno ya tembo.
Aidha alisema ng¡¯ombe 2,663, msumeno mmoja na mbao 745.
Alisema
jumla ya kesi 124 zenye jumla ya watuhumiwa 544 waliojihusisha na
vitendo vya ujangili zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini na
kwamba kati ya hizo, kesi 38 zenye jumla ya watuhumiwa 113 zinaendelea
mahakamani na kesi 62 zenye jumla ya watuhumiwa 85 ziliisha kwa
watuhumiwa kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 25, 510,000.
Hata
hivyo, alisema takwimu za ujangili katika kipindi hicho ikilinganishwa
na kipindi kama hicho kwa mwaka 2014 zinaonyesha kupungua kwa vitendo
vya ujangili kwa asilimia 58, isipokuwa kwa idadi ya meno ya tembo
yanayokamatwa ambayo yanaongezeka kutokana na kukamatwa meno yaliwindwa
siku za nyuma.
CHANZO: NIPASHE
Post a Comment