Mwanafunzi
wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Bangwe Kata ya Bangwe kwenye
Manispaa ya kigoma Ujiji mkoani hapo amepigwa na mwalimu wake katika
maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mguu wa kulia baada ya
kumkatalia kumpa penzi.Akizungumza na mwandishi wetu jana wodi namba 5
katika hospitali ya Rufaa ya Maweni mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kwa
jina la Zubeda Athuman (14) alisema chanzo cha mwalimu huyo kumchukia na
hatimaye kufikia hatua ya kumpiga na kumvunja mguu ni wivu wa
kukataliwa kupewa penzi ,hali iliyomfanya mwalimu huyo kumpa adhabu za
hapa na pale kila aendapo shule.Hali hiyo ilimfanya mwanafunzi huyo
kuwadokeza wazazi wake ambapo walimwambia avumilie,ndipo jumatano ya
wiki hii mwalimu alimpa adhabu ya kuchimba shimo na alikataa kufanya
hivyo baada ya kuona hana kosa la msingi la kumpa adhabu hiyo.
Mwalimu
huyo alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao machi,22,2014 saa 12.30
jioni hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti
alipokwenda shule Machi,24,2014 alimuliza mwalimu huyo sababu ya
kumfuta kwao, hali hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa na
kumpiga vibao vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake
ikiwemo kuvunjika kwa mguu.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Maweni Macris Yakayeshi akiri mwanafunzi huyo
kuvunjika mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo
kwenda upande na wiki ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.
Dr.Yakayeshi
alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo
si chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii
ibadilike na matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai
alifikishwa hapo kifua kikiwa wazi ili hali binti ni rika la balehe na
kuomba sheria ichukue mkondo wake.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo
aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa
adhabu aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia
akamlete mzazi wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza
kumpiga hali iliyolazimu jeshi la polisi kuingilia hekaheka kiyo.
Akizungumzia
tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema alishangaa
kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo
akadai kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu
husika hakuwa muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.
Moshi
alisema baada ya kauli hizo ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na
kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu
ya adha ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata
usiku siku za mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa
alikataa kuwa nae kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zedekia Makunja alipoulizwa kama analifahamu hili akadai naam ila wataitwa machi,31,mwaka huu.
Kwa
nyakati tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya
mwanafunzi juu ya adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto
kwa kuwafundisha adabu ,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na
mwalimu haiwezekani kukataa kwa adhabu amvunje mguu.
Post a Comment