Machafuko
ya hali ya hewa, mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha juu ya
kuwapo kwa kimbunga kiitwacho Hellen katika mwambao wa Bahari ya Hindi
ambacho kitasababisha mvua kubwa inayozidi mililita 50 ndani ya saa 24
kuanzia jana katika mikoa 14
Mamlaka
ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha juu ya kuwapo kwa kimbunga
kiitwacho Hellen katika mwambao wa Bahari ya Hindi ambacho kitasababisha
mvua kubwa inayozidi mililita 50 ndani ya saa 24 kuanzia jana katika
mikoa 14.
Taarifa
ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana kwa vyombo vya habari imebainisha
kuwa mvua zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtara, Lindi, Tanga,
Unguja, Pemba, Singioda, Dodoma, Ruvuma, Katavi, Njombe, Mbeya na
Morogoro.
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa mvua hizo zilitarajia kuanzia jana na zitaendelea
hadi Aprili Mosi mwaka huu na wakazi wa mikoa hiyo, watumiaji wa bahari
pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa zimetakiwa kuchukua tahahadhari
zinazotakiwa.
Imebainisha
kuwa, uwezekano wa mvua hizo ni asilimia 80 na ni mwendelezo wa mvua za
masika zinazoendelea kunyesha nchi nzima katika baadhi ya maeneo ambako
hupata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
“Mamlaka
ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa zaidi kadri
zitakavyopatikana,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa,
uangalifu na tahadhari vinahitajika ili kuepusha maafa zaidi.
Kimbunga
hicho kinakuja wakati baadhi ya maeneo nchini, wiki iliyopita zilikumbwa
na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali
sasa na kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu.
Chanzo;Mwananchi
Post a Comment