Miongoni mwa vitu vilivyoundwa miaka ya hivi karibuni ni Simu ambazo kwasasa ni maarufu sana mtaani. Simu hizi zinazo julikana kama Smartphone zimepelekea mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa teknolojia kwani kupitia simu hii unaweza fanya mambo mengi sana.
Hebu leo tuangalie madhara ya Smartphone kwako wewe mtumiaji.
1. Mmomonyoko wa maadili:Smartphone zimekuwa na ushawishi mkubwa katika kupelekea kushuka kwa maadili kwani simu hizi humrahisishia mtumiaji kuona picha na video mbalimbali zilizopo online. Tafiti zinaonesha kuwa idadi kubwa ya vijana wenye Smartphone kama wewe hapo unaesoma habari hii, hawamalizi wiki moja bila kutazama picha chafu au video iwe ni kwa hiari yao au kuziona kwa bahati mbaya kupitia mitandao ya kijamii.
2. Smartphone pia ni simu ambayo inapelekea watu kupoteza muda mwingi kuchat na marafiki badala ya kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo huenda zingewaongezea kipato chao.
3. Mionzi itokanayo na Simu yoyote ni hatari sana kwa Afya ya mwanadamu kwani wataalamu wanasema kunauwezekano mkubwa wa kupata saratani endapo utaendekeza matumizi ya vifaa vyenye mionzi. Sasa Smartphone ni simu rafiki ambayo humshawishi mtumiaji kuichezea kila siku, kila sasaa na kila mahali endapo una tabia hiyo punguza kwani ni hatari sana....
4. Endapo hautakuwa mwangalifu na mtunzaji mzuri ikatokea siku moja ukaitupia simu yako kwenye majoi basi itakuwa ni kilio na kusaga meno kwani ndo niagieni hiyooo......
USHAURI WA BURE: KAMA UNA SMARTPHONE ITUPE SASA HIVI NA UNUNUE NOKIA TOCHI, Natania tuuu, Ni muhimu kwenda na teknolojia, chamsingi tuzingatie matumizi bora na ya msingi kwenye smartphone zetu na tuweke apps ambazo zitazuia watoto wetu kuzitumia vibaya.
Imeandaliwa na KIJIWE MEDIA, BENCHI LA TEKNOLOJIA
Post a Comment