TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 05.04.2014.
·
MTOTO WA MIAKA MIWILI AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUPIGWA NA MAMA YAKE WA KAMBO.
·
MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI AFARIKI DUNIA AKIWA
ANAOGELEA KATIKA MTO CHAPWA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA BAADA YA KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WATATU KATIKA NYAKATI TOFAUTI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MIAKA MIWILI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANSIS MANENO MKAZI WA ITIMBA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA
MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA MBEYA BAADA YA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE NA MAMA YAKE WA KAMBO AITWAYE HAPPY
PETTER (16) MKAZI WA ITIMBA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.04.2014
MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ITIMBA, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
AWALI MNAMO TAREHE 03.04.2014 MAJIRA
YA SAA 08:00 ASUBUHI MAMA HUYO
ALIMPIGA MTOTO HUYO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUMSABABISHIA MAJERAHA.
CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. UCHUNGUZI ZAIDI
WA TUKIO HILO UNAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI NA JAMII KWA UJUMLA KUTUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA KUWAELEKEZA NA
KUWAKANYA WATOTO BADALA YA KUWAPIGA KWANI NI HATARI NA ZINAWEZA SABABISHA
MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI
KATIKA SHULE YA MSINGI CHAPWA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BLANDA CHARLES (09) AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KWENYE MTO
CHAPWA WAKATI AKIOGELEA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
04.04.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO CHAPWA, WILAYANI
MOMBA, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIKUWA AKIOGELEA
PEKE YAKE NA MWILI WAKE ULIGUNDULIWA NA MMOJA WA WAPITA NJIA AITWAYE KAPANDA
CHISUNGA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA UKISUBIRI
KUSAFIRISHWA KWENDA MBEYA KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO
WAO, KUTOWARUHUSU KUFIKA/KUKARIBIA MAENEO YENYE MAJI KAMA VILE MITO NA MABWAWA
WAKIWA PEKE YAO KWANI NI HATARI KWA MAISHA YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII
KUFUNIKA VISIMA PAMOJA NA KUFUKIA MASHIMO MAKUBWA YALIYOPO KATIKA MAENEO YAO
KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASANJA JOHN
(32) CLEARING AGENT, MKAZI WA MTAA
WA MWAKA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA GARI LENYE
NAMBA IT 9446 AINA YA TOYOTA PRADO AMBALO NI MALI YA
WIZI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.04.2014
MAJIRA YA SAA 15:45 ALASIRI HUKO
KATIKA MTAA WA MAJENGO – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA,
MKOA WA MBEYA.
AWALI MNAMO
TAREHE 16.12.2013 GARI HILO LILIKUWA
LINASAFIRISHWA KUTOKA DSM KUELEKEA LUSAKA ZAMBIA NA NDIPO LILIIBWA LIKIWA
LIMEPAKI KATIKA HOTELI YA SILVER STONE TUNDUMA. THAMANI HALISI YA GARI HILO NI TSHS 21,775,000/=.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHANA NA TAMAA ZA UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA ZISIZO HALALI NA BADALA YAKE
WATAFUTE MALI KWA NJIA HALALI KWA KUJISHUGHULIA KATIKA KAZI HALALI.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA FAINES MSOMBA (32) MKAZI WA MAWELO NA DAINES ASWILE (28) MKAZI WA MAKONGOLOSI
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
UJAZO WA LITA 21.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:00
MCHANA KATIKA MAENEO TOFAUTI, MTUHUMIWA WA KWANZA ALIKAMATWA KATIKA
KITONGOJI CHA MAWELO, KIJIJI CHA MNAZI MMOJA, KATA YA MAWELO, TARAFA YA KIWANJA
WAKATI MTUHUMIWA WA PILI ALIKAMATWA KATIKA MTAA WA TRM – MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI,
TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE
HIYO HARAMU, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MARIAM ASAJILE (42) MKAZI WA KYIMO NA 2. ASWILE
MWAKIBASA (20) MKAZI WA KIJIJI CHA KALALO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05].
WATUHUMIWA
WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 04.04.2014 MAJIRA YA SAA 18:00
JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA
RUNGWE MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI/WAUZAJI WA POMBE
HIYO, MARA TARATIBU ZITAKAPO KAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
MSAKO WA TATU, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FELEX GEOFREY (20) MKAZI
WA KIWIRA – TUKUYU ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE
KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SEIKALI AINA YA
BOSS KATONI 30 ALIZOKUWA AMEPAKIZA KWENYE PIKIPIKI YAKE YENYE NAMBA ZA
USAJILI T.514 CRD AINA YA T-BETTER.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA
MNAMO TAREHE 04.04.2014 MAJIRA YA
SAA 13:30 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI
CHA NGANA, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA MARA MOJA KUJISHUGHULISHA NA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA
MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA ZINA MADHARA KWA AFYA YA
MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment