Gari la magazeti la kampuni ya The Guardian ambalo limetua Iringa hivi sasa saa 2.40 Asubuhi hii baada ya kupona kutekwa MAJAMBAZI
ambayo idadi yao haikufaanika mara moja usiku wa leo wamefunga
barabara ya Morogoro -Iringa eneo la Doma na kufanya unyama wa
kutisha kwa wasafiri wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na
kuwalazimisha kufanya mapenzi wanaume kwa wanaume na kuwatesa vibaya
madereva kabla ya kuwapora mali zao . Miongoni mwa walioteswa na pamoja na rasta dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya globalpublishers
ambae anadaiwa kujeruhiwa mkono wake huku dereva wa gari la
magazeti ya kampuni ya Mwananchi akinusurika na gari lake kupinduka
wakati akikwepa vizuizi vya magogo vilivyotegwa barabarani. Wakizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com asubuhi ya leo mjini Iringa
wahanga wa tukio hilo Ally Malinda (44) mkazi wa Itunda Dar es Salaam
na Rashid Yusuph Kahese (37) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam
ambao kwa pamoja wanaendesha gari ya magazeti ya kampuni ya The Guardian
walisema kuwa tukio hilo lilmetokea mida ya saa 8 usiku wa leo
hadi saa 11 Alfajiri baada ya watekaji hao kuachia mateka hao . Malinda
alisema kuwa kabla ya kufika eneo ambalo watekaji hao walikuwa
wamewateka abiria wengi zaidi walikutana na makundi ya watu
waliotekwa na kuporwa ambao walikuwa wakiwasimamisha wasiendelee
na safari ila hawakusimama wakijua ni wezi . " Tulienda mbele
kidogo tukakutana na kundi jingine ila bado tulipuuza na kupita baada
ya kufika mbele ndipo tuliona magari yakiwa yamegeuka huku na
kule huku wengine wakiteswa na ndipo tulipofanikiwa kugeuza gari
letu lenye namba za usajili T 812 CNZ na kukimbia . Hata hivyo
alisema polisi Morogoro walipigiwa simu ila hawakuweza kufika hadi
majira ya saa 11 Alfajiri watekaji hao walipoamua kuwaachia mateka. "
Kila tukimpigia kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro aliishia kusema
kuna askari wametumwa kuja eneo la tukio ila hadi asubuhi hakuna
askari aliyefika .....na majeruhi wamepelekwa Hospital ya mkoa wa
Morogoro kwa matibabu zaidi" Mtandao huu wa matukiodaima .com
unaendelea kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro ili
kuzungumzia tukio hilo zaidi .chanzo;francis godwin blog |
Post a Comment