Kaimu
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia bi Prisca Ulomi akitoa wito kwa wananchi
kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salam . Kaimu
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi akiwaeleza waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika
Uandaaji wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mtandao,kushoto ni Afisa
habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
……………………………………………………………………….
Fatma Salum-Maelezo
Serikali
yawatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuondoa vitendo vya uhalifu hapa
nchini.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Prisca
Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam.
Akifafanua
Bi Prisca amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa
kutambua umuhimu wa TEHAMA wameamua kuandaa muswada wa Sheria za
Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao (Cyber Laws).
Akieleza
zaidi Bi Prisca amesema kuwa Muswada wa sheria hizo ni pamoja na
Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data
Protection Bill), Muswada wa Sheria ya Biashara ya Miamala ya
Kielektroniki (Electronic Transaction Bill), na Muswada wa Sheria ya
Kuzuia Uhalifu kwa njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber
Crimes Bills).
“Sheria
hizo zitasaidia kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano hapa nchini kwa kudhibiti uhalifu kwa kutumia mitandao na
kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya mitandao”. alisema Bi
Prisca.
Bi
Prisca aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuweka
miundombinu ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha na kuharakisha utoaji
wa huduma mbalimbali na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatumia
vibaya teknolojia hiyo, hivyo kunaumuhimu wa kuwepo sheria zitakazodhibiti uhalifu kupitia mitandao.
Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imetoa rai kwa wananchi
kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri
mitandao hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hali inayoweza
kuathiri ukuaji wa sekta hiyo nchini.
Post a Comment