0


Afisa wa vipimo katika Idara ya Ardhi Manispaa ya Lindi Bi. Kisna Mgeni akitoa maelezo kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour wakati alipozindua mradi wa Upimaji wa Viwanja katika Eneo la Ngongo, Leo May 22,2017 Mkoani Lindi.Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Joomary Satura akitoa maelezo kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour wakati alipozindua mradi wa Upimaji wa Viwanja katika Eneo la Ngongo, Leo May 22,2017 Mkoani Lindi.
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
KATIKA kuhakikisha inavutia wawekezaji na kufikia azma ya kushiriki kukuza uchumi wa viwanda. kwa mtendaji wa halmashauri hiyo, Joomary Satura, wakati wa uwekeji jiwe la msingi mradi huo uliopo maeneo ya Ngongo na Ngurumahamba.
Halmashauri hiyo imetenga eneo la viwanda vidogo na vikubwa katika maeneo ya Ngurumahamba. Ambapo viwanda vya kubangua korosho, kutengeneza magunia, na kutengeneza dawa aina ya salfa vimepimwa.
“Sera ya ardhi ya mwaka 1995 imeeleza bayana kwa kuzitaka halmashauri kutenga maeneo maalum kwa ajili ya viwanda na uwekezaji, pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali” Manispaa ya Lindi tunatekeleza sera hii kwa vitendo,” alibainisha Satura.
Alizitaja baadhi ya faida ya mradi huo ni kudhibiti ujenzi holela wa makazi, kuongeza hadhi ya viwanja vya maonesho ya NaneNane kwa kusogeza huduma mbalimbali za kijamii, kuongeza mapato ya halmashauri na serikali kuu.
Faida nyingine ni kuongeza ajira, kurahisisha upatikanaji wa soko la mazao na kuongeza chachu ya viwanda vingine vikubwa na vidogo. Uwekaji wa jiwe la msingi mradi huo ulikwenda sanjari kukabidhi hati miliki tatu za ardhi kwa bodi ya korosho ambayo ni mwekezaji wa kiwanda cha magunia, kubangua korosho na kutengeneza dawa ya unga aina ya salfa
.

Post a Comment

 
Top