Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifatilia taarifa za Kata kwa makini
Baadhi ya Wataalamu walioshiriki kwenye kikao cha Baraza
Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya akitoa pongezi kwa watendaji wa Manispaa kwaniaba ya Madiwani wote.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba akitoa taarifa ya kupokea Hati safi kutoka CAG
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad akiwapongeza Wataalamna Madiwani kwa ushirikiano uliopelekeakupatikana kwa Hati safi.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni limeipongeza Manispaa kwa kupata Hati safi baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba kutoa taarifa ya kupokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG )inayoonesha Manispaa kuwa na hati safi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Pongezi hizo zimetolewa leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la kawaida la robo ya tatu ya mwaka (Jan-Mach 2018) lililofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Kisota .Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad amesema kuwa Hati safi imepatikana kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Wataalamu wa Manispaa na Madiwani na kwamba ni faraja kwa Manispaa nzima.
"Tumefarijika sana kupata matokeo haya, hati hii safi isingepatikana kama kungekuwepo na kutokuelewana baina ya wataalamu na madiwani, tunajivunia umoja wetu"Alisema Mh.Hoja .Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya amesema kuwa kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Baraza lina kila sababu ya kuipongeza Manispaa kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha pamoja na upya wake hati safi inapatikana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa tafsiri ya matokea haya ni ushirikiano uliopo kati ya watendaji , wasimamizi pamoja na Waheshimiwa Madiwani ndio uliopelekea kupatikana kwa Hati safi.
Ameongeza kuwa kuangalia nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali, kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba rasilimali watu ambao anawaongoza wapo katika kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa la wananchi kupata huduma zile zilizokusudiwa. Tunashukuru tumeweza kufikia malengo yaliyotarajiwa na tunaamini hata katika mwaka wa fedha unaokuja tutaendelea kufanya vizuri" Alisema Mkurugenzi.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepata hati safi ( Unqualified Report) kwenye sekta zote na miradi ya maendeleo ikiwemo ya Barabara na Maji inayotekelezwa na Manipsaa
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
04/05/2018.
Post a Comment