0
WillianHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBao la Willian kipindi cha pili lilikuwa lake la 11 kufungia Chelsea mashindano yote msimu huu
Klabu za Chelsea na Barcelona zimemetoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 16 katika michuano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya UEFA.
Katika mchezo huo Chelsea ndiYo walikuwa wa kwanza kufunga bao la dakika 62 kipindi cha pili likifungwa na Willian Borges Da Silva kufutia pasi ya Eden Hazard.
Muda mfupi baadaye Barcelona wakafanikiwa kusawazisha bao hilo mnamo dakika ya 75 kipindi cha pili lililofungwa na Lionnel Messi kufuatia pasi ya Andrea Iniesta.
Timu hizo zitarudiana tena mwezi Machi katika dimba la Nou Camp.
Chelsea yatoa sare ya 1-1Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionChelsea yatoa sare ya 1-1
Katika mchezo mwingine Bayern Munich waliwakaribisha Besktas, mchezo huo umemalizika kwa Bayern Munich kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, mabao ya Bayern yamefungwa na Thomas Muller, Kingsley Coman na Robert Lewandowski. Michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya inaendelea tena leo Jumatano kwa michezo miwili, Sevilla wanawaalika Manchester United na Shakha Donestk ni wenyeji wa As Roma.

Post a Comment

 
Top