0
*Ataka takwimu za kahawa ziwe tayari ifikapo Feb. 28

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji na Wilaya za Mbinga wahakikishe kuwa wanaunda kanda za kilimo na kuwasambaza maafisa kilimo wao badala ya kuwaacha wakae maofisini.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Ijumaa, Januari 5, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga, kwenye ukumbi wa Jumba la Maendeleo, mjini Mbinga.

“Mkurugenzi wa TC na DC chuja maafisa kilimo ulionao na uhakikishe wanabakia watatu tu. Abaki DALDO, mtu wa horticulture na mthamini, wengine wote wasambaze kwenye kanda ili wasimamie wakulima wakiwa huko huko. Hili litekelezwe na Mkuu wa Wilaya ulisimamie” alisema.

Aliwataka maafisa kilimo wa zao la kahawa waende vijijini na kufanya sensa ili waweze kubaini wana wakulima wangapi wanaozalisha kahawa. “Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue kijiji kina wakulima wangapi wa kahawa, na wana ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana miche mingapi? Hii itaisaidia Serikali ijue inahitaji dawa za aina gani, mbolea kiasi gani na miche mingapi kwa wakulima wake,” alisema.

“Ninataka hizi takwimu ziwe zimekamilika ifikapo tarehe 28 Februari, mwaka huu,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mche wa Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo. Januari 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kitalu cha miche ya Kahawa, wakati alipotembelea kituo cha utafifti wa zao la kahawa (TACRI) kilichopo kwenye kijiji cha Ugano Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Dkt. Deusdedit Kilambo na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Januari 5, 2018
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia kahawa kwenye mashine ya kusagia kahawa, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kushoto ni Meneja Uzalishaji Rabiel Ulomi na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Januari 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia sampuli za kahawa kwenye, wakati alipotembelea kiwanda cha kahawa cha Mbinga Coffee kilichopo Mbinga Mjini Wilayani Songea, Mkoani Ruvuma, kulia ni Meneja Uzalishaji Rabiel. Januari 5, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Watumishi wa Halmashauri ya Mbinga, Mkoani Ruvuma, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Ruvuma. Januari 5, 2018.

Post a Comment

 
Top