0
Benki kuu Tanzania yafunga jumla ya benki tanoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBenki kuu Tanzania yafunga jumla ya benki tano
Benki kuu nchini Tanzania imefuta leseni za benki tano na kuziweka chini ya mrasimu.
Benki kuu ilisema benki hizo zinakumbwa na matatizo ya kifedha.
Ilisema kuwa benki hizo kuendelea kuhudumu katika hali zilivyo sasa inaweza kuwa hatari kwa mifumo ya kifedha.
Covenant Bank for Women, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Meru Community Bank Limited, na Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited zote zimepoteza leseni zao.
Sambamba na benki hizo, pia benki tatu zimewekwa katika kipindi cha mpito cha miezi 6 kuweza kukidhi kiwango elekezi cha mtaji wa shilingi bilioni 2( dola za Marekani laki tisa) vingenevyo zitafungwa.
Kufungwa kwa benki hizi kuna maanisha kwamba wapo watakaopoteza amana zao, kwani bodi ya bima ya amana italipa kiwango elekezi pekee ambacho ni shilingi za Tanzania milioni 1.5 pekee (dola za Marekani 700). Hii ni kwa mujibu wa Beno Ndulu, aliyekuwa gavana mkuu wa benki kuu Tanzania.
Professa Florence Luwoga,(kushoto) Gavana mpya wa Benki Kuu Tanzania akiambatana Professa Beno Ndulu aliyekuwa gavana mkuu wa benki kuu nchini humo, wakizungumza na waandishi wa habari.
Image captionProfessa Florence Luwoga,(kushoto) Gavana mpya wa Benki Kuu Tanzania akiambatana Professa Beno Ndulu(kulia) aliyekuwa gavana mkuu wa benki kuu nchini humo, wakizungumza na waandishi wa habari.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi, ya kumtambulisha gavana mpya wa benki kuu, alisema uchumi wa Tanzania bado uko imara na kushuka kwa uwezo wa mabenki kukopesha si kigezo cha kushuka kwa uchumi kwani wawekezaji wakubwa wanaotegemewa na nchi hiyo, wanapata mitaji yao kutoka nje.
Gazeti la The East African linasema kuwa wiki tatu zilizopita, Rais John Magufuli aliamrisha benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zisizo na fedha za kutosha.
Wachumbuzi wa maswala ya kiuchumi wanakinzana na kauli ya gavana. Katika mahojiano na BBC, mchambuzi wa uchumi, Betty Masanja amesema kuwa kusinyaa kwa sekta binafsi ndiyo sababu ya mabenki kuanguka kimtaji huenda hali hii ikaendelea kutokana na mzunguko wa fedha kuwa finyu.

Post a Comment

 
Top