0
Odinga
Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya leo Jumanne, baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.
Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi. Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.
Idara ya Polisi nchini humo tayari imepiga marufuku kufanyika kwa zoezi hilo hii leo.
Inakisiwa kuwa idadi kubwa ya wafuasi wa upinzani, wamesafiri usiku kucha kutoka maeneo ya mbali ili kufika Nairobi kwa sherehe hizo.

Post a Comment

 
Top