0
                                                  


Leo January 8, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ametangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika November 22 na 23, 2017, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Dr. Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Wanafunzi wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kwa upande wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya wanafunzi 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde ametangaza wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Post a Comment

 
Top