0
Manchester City yamsajili beki Aymeric Laporte katikati kwa kitita kilichovunja rekodiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester City yamsajili beki Aymeric Laporte katikati kwa kitita kilichovunja rekodi
Klabu ya Manchester United imemsajili beki wa Ufaransa Aymeric Laporte kutoka Athletico Bilbao kwa kitita kilichovunja rekodi ya timu hiyo cha £57m.
Kitita hicho cha Laporte ambaye hajaichezea timu ya taifa ya Ufaransa , kinajumlisha gharama ya vilabu vya Uingereza mwezi huu kufikia £252m ikiwa ni rekodi katika uhamisho wa mwezi Januari.
Kuwasili kwa mchezaji huyo ,mwenye umri wa miaka 23 kunajumlisha gharama ya klabu hiyo kuwanunua mabeki tangu mwisho wa msimu uliopita kufika £215.5m.
Yaya Toure, kigogo wa Manchester City
Rekodi ya awali iliwekwa na kiungo wa kati wa klabu hiyo Kevin de Bryune aliyenunuliwa kwa kitita cha £55m 2015.
''Ninatazamia kufanya kazi chini ya mkufunzi Pep Guardiola na kujaribu kuisaidia klabu hiyo kupata ufanisi, aliambia mtandao wa klabu hiyo. Inamaanisha kwamba klabu hii imeniamini na nafurahia kushirikiana nayo''.
Wasiwasi kuhusu jeraha la beki Vincent Kompany mbali na wasiwasi mwengine kuhusu kutokuwepo kwa Eliaquim Mangala kumemshinikiza Guardiola kuamini anahitaji beki mwengine wa kati mbali na John Stones na Nicolas Otamendi.

Post a Comment

 
Top