0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli bado anaendelea kushika headlines tokea mkoani Dodoma ambapo leo December 14, 2017 amefungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania na kuwataka Watanzania kuwajibika na kuacha kulalamika kuwa vyuma vimebana.“Watu wanasema vyuma vimebana, weka grisi vyuma havitabana, wengi wanaosema vyuma vimebana ni hawa waliokuwa wanapata hela za mishahara hewa, wafanyakazi hewa, mikataba hewa, wale vyuma vitabana sio kubana tu vitavunjika,” – JPM
“Hatuwezi tukaiacha Nchi ikaendelea kuchezewa wakati wapo wafanyakazi wengine wanaohangaika, walimu wanahangaika kwa ajili ya Watanzania wa maisha ya kawaida, lazima twende pamoja kwa maslahi ya nchi yetu, nataka niwaambie walimu toka kwenye moyo wangu nawapenda,” – JPM
“TANZANIA IMESHAONEKANA KUWA NI KICHAKA CHA FEDHA ZA KIGENI” JPM, BONYEZA PLAY  HAPA CHINI KUTAZAMA

Post a Comment

 
Top