Kutokana na korosho kutokuwa na ubora imesababisha zaidi ya tani 300 kukosa mnununzi katika ghala la nangurukuru lilipo wilayani kilwa.
MENEJA rasilimali watu na utawala SHAURI MOKIWA amevitaka vyama vya msingi kutopokea korosho ambazo hazina ubora kwani kunasababisha baadhi ya wanunuzi kuzikwepa korosho hizo na matokeo yake bei hushuka .
BI MOKIWA ameyasema hayo kwenye mnada wa 8 uliofanyika katika kijij cha kiwalala halmashauri ya lindi ambapo kutokana na korosho kutokuwa na ubora kumesababisha korosho kuuzwa bei ya juu kwa sh.3790 na ya chini 3767 ambapo maghala yaliyouzwa ni ghala la buko manispaa na ghala la mtama halmashauri ya lindi .
MOKIWA ameeendelea kusema kuwa wakulima waweke pesa wanazozipta ilikuweza kununulia pembejeo na kutotegemea serikali ambapo km mwaka huu pembejeo zilichelewa na matokeo yake baadhi ya wakulima wanauza korosho ambazo hazina ubora kutokana na kuchelewa kupulizia mikorosho yao.
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa lindi mwambao OMARY CHIPATU amesikitishwa kwa ghala la nangurukuru kukosa mnunuzi na kuamua korosho zilizobaki kuuzwa mnada ujao
Post a Comment