0
Klabu ya Simba yenye maskani yake jijini Dar es Salaam katika Mtaa wa Msimbazi kupitia Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club Haji Manara imebainisha kuwa Klabu hiyo imeamua kuachana na Kocha wake Joseph Omog.Kupitia taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Mtandao wa Instagram wa Manara inasema kuwa Klabu na OMOG wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalumu yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Aidha taarifa hiyo imeonyesha kumshukuru kocha huyo na kumtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya nje ya Simba.
Kwa sasa Klabu hiyo itakuwa chini ya mkufunzi Msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi siku ya kesho na kupumzika siku ya jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya kusafiri kwenda Mtwara kwa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ndanda.
Kupitia Taarifa hiyo Uongozi wa Simba umetumia nafasi hiyo luwaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa matokeo mabaya ya hapo jana. Wamewataka mashabki kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu katika klabu yao.

Post a Comment

 
Top