![]() |
Afisa
Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza akiongea
na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la
kisasa la Tigo wilayani humo.
|
![]() |
| Baadhi ya wakazi na Biharamulo wakifuatilia uzinduzi wa Duka jipya la kisasa la Tigo |
![]() |
| Meneja Mauzo wa Tigo Biharamulo, Abraham Mchau akiongea na waandishi na wakazi wa Biharamulo waliohudhuria uzinduzi wa duka la kisasa la Tigo wilayani humo. |
![]() |
| Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo. |
![]() |
| Afisa Mauzo wa Duka hilo, Lucy Ernest akifafanua jambo kwa Afisa Habari na Mawasiliano wilaya ya Biharamulo, Jonathan Rwekaza kuhusu bidhaa mbalimbali ndani ya duka jipya la Tigo Biharamulo. |
![]() |
| Picha ya pamoja |
Biharamulo, 7 Desemba, 2017- Katika
mwendelezo wa harakati za kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanapata
huduma bora kwa urahisi, kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali
Tigo Tanzania leo imezindua duka kubwa la kisasa wilayani Biharamulo
katika Mkoa wa Kagera.
Duka
hilo jipya linapatikana katika Jengo la Yusuph Katri lililopo Stendi ya
Mabasi ya Biharamulo, mkabala na Kituo cha Polisi na lina uwezo wa
kuwahudumia wateja zaidi ya 700,000 wa Tigo wanaopatikana wilayani hapo
na viunga vyake.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kuzindua duka hilo jipya la Tigo, Meneja Mauzo wa
Tigo - Biharamulo, Abraham Mchau alisema kuwa ufunguzi wa duka hilo
jipya unaendana na mpango wa upanuzi na ukuaji wa kampuni hiyo ya simu
unaolenga kuongeza idadi ya vituo vya huduma kwa wateja huku
ikihakikisha kuwa bidhaa na huduma zote zinapatikana kwa urahisi na
wateja wake nchi nzima.
‘Tigo
imejizatiti kufanya uwekezaji utakaohakikisha wateja wetu wanapata
huduma kwa viwango vya kimataifa ili waweze kupata suluhisho muafaka kwa
mahitaji yao. Ufunguzi wa duka hili la kisasa mjini Biharamulo
kunafanya idadi ya maduka yetu ya Tigo kufikia 15 katika Ukanda huu wa
Ziwa, huku jumla ya maduka yetu yote ya Tigo nchini ikifikia 75,’
alisema.
‘Uzinduzi
huu unaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa zaidi wateja
wake na kuwapa bidhaa na huduma bora, za kibunifu, zinazoendana na
mahitaji yao. Tunaendelea kuwekeza katika upanuzi na uboreshaji wa
mtandao wetu wa simu, ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anakuwa sehemu ya
mabadiliko na faida za ulimwengu wa kidigitali unaoongozwa na Tigo,’
Mchau alifafanua.
Kwa
upande wao, wakaazi wa Biharamulo wameelezea kufurahishwa kwao na ujio
wa duka hilo jipya la Tigo kwani litawapunguzia adha ya kusafiri kwa
mwendo mrefu kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya simu pamoja na kuboresha
upatikanaji wa huduma za simu katika wilaya hiyo.







Post a Comment