Mahakama nchini Misri inaripotiwa kumfunga mwimbaji mmoja miaka miwili jela baada ya kuonekana kwenye video moja ya mziki akiwa na vazi la ndani huku akila ndizi.
Shaimaa Ahmed, 25, ambaye kimuziki anafahamika kama Shyma, alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo.
Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.
Mwelekezi wa video pia naye alihukumua kifunga cha miaka miwili licha ya yeye kutokuwepo mahakamani.
Shyma alikuwa ameomba msamaha kabla ya kukamatwa.
"Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwaa kwa njia hii kali kutoka kwa kila mtu."
Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngono kwenye video ya muziki.
Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.
Chanzo- BBC
Post a Comment