Ushiriki mdogo wa jamii katika masuala ya utetezi wa watoto ni moja ya changamoto zinazokwamisha juhudi za kutatua matatizo ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ,unyanyasaji na mimba za utotoni.
Haya yamebainishwa na Mkurugenzi ,,, wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Lindi
Jesca Haule Mkurugenzi wa OWE alisema ushiriki mdogo wa jamii katika kujihusisha na utetezi wa kukabiliana na matatizo ya ukatili wa kijisia, kuficha taarifa na matendo ya ukatili vinapo tokea ikiwemo matendo ya ubakaji kwa watoto wa kike, mimba za utoto kwani wazazi wamekuwa kikwazo hasa pale wanaposhirikiana na watuhumiwa kuficha watuhumiwa kwa kuwataka wasichana wasiwataje kwani inakwamisha kutafuta ufumbuzi , tiba sahihi ya tatizo.
Kwa upande mgeni rasmi wa tukio hilo mkuu wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewata wanajamii wakiwemo wazazi kutoa ushrikiano wakati wanapotakiwa kufanya hivyo ili kutomeza matendo ya ukatali wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Ndemanga alisema amewataka wananchi wa wilaya Lindi kuacha tabia ya kutumia fedha za korosho vibaya kwa kunyanyasa wanawake na watoto ikiwemo tabia ya kutoshirikisha kwenye mapato na matumizi yake
Post a Comment