SIMBA imemleta beki Mghana, Malik Ismaila wa Tema Youth ambaye pia anakipiga katika timu ya taifa ya chini ya miaka 23.
Beki huyo alitua juzi Jumamosi kwa ajili ya mazungumzo na Wekundu hao jambo linaloashiria kuna staa mmoja wa kigeni atakwenda na maji siku si nyingi.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema mchezaji huyo mwenye kimo kama cha Juuko Murshid, ana nafasi kubwa ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo anayekwenda Gor Mahia ya Kenya kwa mkopo.
Ujio wa mchezaji huyo aliyefikia hotelini Kariakoo, unamaanisha Joseph Omog lazima afanye maamuzi magumu kama bado ana msimamo wa kumsajili straika wa Rayon ya Rwanda, Shazir Nahimana.
KUANGALIA TETESI ZA USAJILI WA YANGA BOFYA >>HAPA<<
KUANGALIA TETESI ZA USAJILI WA YANGA BOFYA >>HAPA<<
Post a Comment