Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHuu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza mwaka 1976
Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo leo wameanzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.
WHO linasema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamkaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.
Huenda watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza leo watakaopewa chanjo hiyo ya majiribio.
Awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano.
Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016 katika Afrika ya magharibi.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionUgonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, kati ya mwaka 2014-2015.
Dalili za Ebola
Dalili za Ebola ni homa, kufuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.
Maafa ya ugonjwa huu huweza kufika asilimia tisini - lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa 55% .
Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.
Hakuna kinga wala tiba
Huduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kupona
Inafikiriwa kuwa popo ndio hubeba virusi vya ugonjwa huo.
Ufanisi wa Chanjo ya Ebola
Uchunguzi uliofanyiwa chanjo ya ugonjwa wa Ebola mwaka jana umebaini kuwa inaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kwa takriban mwaka mmoja.
Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500.
Wale waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Ki...Read more »
kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa...Read more »
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHuenda ndege zikatengezwa bila madirisha katika siku za usoni.
Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua nd...Read more »
Image captionMaandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu tuhuma za ubakaji katika shule ya Moi Girls Nairobi
Walimu pamoj...Read more »
Operesheni ya mwisho ya Tundu Lissu imefanyika na kumalizika salama.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alifanyiwa op...Read more »
Haki miliki ya pichaAFPImage captionBado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.
Bunge nchini Rwanda...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.