Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo, 32, amefanya mazungumzo ya siri na PSG (DiarioGol, in Spanish)
Alan Pardew anatarajiwa kuteuliwa kuwa mkufunzi mpya wa West Brom na inatarajiwa kwamba mkufunzi huyo wa zamani wa Crystal Palace huenda akaanza kazi siku ya Jumatatu.. (Sun)
Kiungo wa kati wa Ujerumani na Arsenal Mesut Ozil, 29, atapewa mkataba wa dau la £350,000 kwa wiki ili kuhamia Barcelona (Daily Mirror)
Lakini mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amekana kwamba hakuna mazungumzo yoyote ya Ozil kuondoka katika klabu hiyo ya uwanja wa Emirates (Daily Star)
Mkufunzi Antonio Conte anaitaka Chelsea kusuluhisha swala la kandarasi mpya ya kipa Thibaut Courtois. (Guardian)
Vyombo vya habari vya Ubelgiji vinadai kwamba Courtois, 25, anataka kulipwa Yuro 230,000 kwa wiki (£205,000) ili kupata mshahara sawa na kipa David de Gea katika klabu ya Manchester United. (HLN, in Dutch)
Mkufunzi wa zamani wa West Brom Tony Pulis anaongoza orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuchukua wadhfa wa ukufunzi katika klabu ya Swansea City iwapo mkufunzi Paul Clement atafutwa. (Daily Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 23,ameripotiwa kukubali kandarasi na klabu ya ligi ya serie A Juventus (Tuttosport, via Daily Star)
Fiorentina imeingia katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 20 Henry Onyekuru, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Anderlecht. (Sun)
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anasema kuwa atajadiliana kuhusu uhamisho na mkufunzi Arsene Wenger wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguliwa katika kipindi cha wiki chache zijazo kwa kutochezeshwa katika ligi ya Uingereza. (Daily Express)
Mwenyekiti wa Everton Farhad Moshiri amewaorodheshwa wakufunzi watatu na ametangaza kuwa hivi karibuni watamuajiri kocha wa klabu hiyo.(Reuters)
Post a Comment