Aliyekuwa waziri wa fedha nchini Zimbabwe Ignatius Chombo ambaye alikuwa amekamatwa na jeshi baada ya kuchukua mamlaka amewasilishwa mahakamani.
Anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka wakati alipokuwa waziri wa serikali za mitaa, wakili wake amesema.
Bwana Chombo ni miongoni mwa maafisa wakuu wa serikali waliokamatwa baada ya rais Mugabe kuzuiliwa nyumbani kwake mnamo tarehe 14 Novemba.
Kwengineko , mahakama kuu imeamuru kwamba unyakuzi wa mamlaka uliotekelezwa na jeshi ulikuwa wa halali.
- Mugabe: Mambo 5 unayopaswa kuyafamu
- Makamu wa rais wa Zimbabwe akataa kurudi nyumbani
- Mugabe na mkewe wasusia sherehe ya kuapishwa kwa Mnangagwa
Hatua ya jeshi kuzuia kujilimbikizia mamlaka kwa wale waliokuwa karibu na Robert Mugabe ni kinyume na katiba, kituo cha habari cha kitaifa nchini Zimbabwe kiliinukuu mahakama hiyo.
Mahakama hiyo pia iliamua kwamba ilikuwa kinyume na sheria kufutwa kazi kwa aliyekuwa makamu wa rais ambaye sasa ni rais mpya wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa mwezi huu.
Hatua ya jeshi kuchukua mamlaka ilionekana kuwa jibu la rais Mugabe kumwachia madaraka mkewe kwa lengo la kumrithi na dhidi ya hatua ya Mnangagwa kufutwa kazi.
Mahakama kuu ilisema katika uamuzi wake kwamba hatua hiyo itawazuia watu ambao hawajachaguliwa kutumia madaraka ya wale ambao wamechaguliwa.
Post a Comment