Shirika la viwanda vidogovidogo SIDO kwa Kushirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa Lindi linatarajia kufanya Maonesho ya biashara kwa kukutanisha wajasirimali zaidi 3000 wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro , Pwani na Ruvuma.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Meneja wa Sido Lindi Salma Ally alisema maonesho haya yanatarajia kuanza tarehe 6 Novemba hadi tarehe 12 Novemba 2017 yakiwa na lengo la kukutanisha wajasiriamali , ili kubadilishana uzoefu na mbinu za kibiashara na elimu ya mikopo.
Salma Aliongeza kwenye maonesho hayo taasisi mbalimbali za umma zitatoa elimu kwa wajasiriamali namna ya kutumia frusa za mikopo, elimu na teknolojia mbalimbali.
Aidha amewataka wananchi mkoani Lindi kuungana na wajasiriamali wengine kushiriki maonesho hayo ili kujifunza na kutumia frusa mbalimbali zitakazo tolewa ikiwemo elimu ambayo itawasaidia kuimarisha ushindani wa soko na kuwaleta pamoja wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale wanaochipukia ili kupata fursa ya kuuza, kuonesha na kujadili masuala ya biashara kwa ujumla.
Aliongeza kuwa SIDO inalenga kusaidiana na serikali katika kutimiza malengo ya milenia likiwemo kuondoa umasikini, na kutoa frusa kwa wajasiriamali kuonesha na kuuza bidhaa zao
Post a Comment