0
Mchezaji wa timu ya New Boys akimiliki mpira kwenye mchezo dhiya Leopard fc 

Matokeo ya mchezo wa hatua ya robo fainali ligi ya Alizeti cup 2017 kati ya New Boys fc dhidi Leopard fc lep oktoba 16 umemalizika kwa timu ya Leopard fc kuibuka na ushindi wa magoli 5 kwa 1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Leopard fc ilifanyikiwa kuongoza magoli 3 kwa bila na kipindi cha pili waliweza kuongeza magoli 2 huku timu ya New Boys ilipata goli moja.

Magoli 4 ya Leopard fc yalifungwa na Lawrance Fusi namo dakika ya 24,32,52,69 na goli la tano likifungwa na Abuu Kazumari na goli moja pekee la New Boys likifungwa na Mohamedi Mtila katika dakika ya 86.

Baada ya mchezo huu kumalizika tulizungumza na msemaji mkuu wa timu ya New Boys,Isa Mbenu aliseme hali ya uwanja imechangia kuweza kufungwa katika mchezo na alishauri uwongozi wa tff kuweza kuliangalia suala lakuweza kuboresha uwanja kabla ya mashindano na kocha wa Leopard fc,Zuberi Nyanga alisema licha ya kuibuka na ushindi lakini mchezo huo ulikuwa mgumu na aliweza kutoa salamu kuwa hakuna timu anayoiogopa kibwa yeye ataendelea kutoa dozi tu.

kesho oktoba 17 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Mitumba fc dhidi ya Super stars fc.

Kuangalia ratiba ya michuano hii bofya >>HAPA<<











Post a Comment

 
Top