0

Chingulungulu Cup 2017
Masasa-Mtwara
Ligi ya Chingulungulu cup imeanza kutimua vumbi rasmi leo octoba 4 kwa mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya New Boys Vs Stone fire na mchezo huo umemalizika kwa sare ya goli 1-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Hifadhine studium.

Katika kipindi cha kwanza timu ya New Boys ilikuwa ya kwanza kufumani nyavu mapema namo dakika ya 32 lilofungwa na Leornad Tunda na Stone fire waliweza kusawazisha goli hilo dakika ya 81 kupitia mchezaji wao Akiba Selemani.

Timu zilizothibisha kushiriki ligi ya Chingulungulu ni 10 ambapo ligi hiyo mshindi wa kwanza atajishindia fedha taslimu shilingi 300,000 na mshindi wa pili atakabiziwa mbuzi na mshindi wa tatu atapata fedha shilingi 30,000.

Kesho octoba 5 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Cardiff fc Vs Namalembo fc

Post a Comment

 
Top