
Kipa namba moja wa Yanga, Youthe Rostand amesema baada ya ushindi dhidi ya Njombe, sasa timu yao inakwenda vizuri na wataimarika kadri siku zinavyokwenda.
Rostand ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitoka African Lyon, alisema timu yao ilianza kwa kusuasua lakini baada ya ushindi wa juzi Jumapili mambo yatabadilika.
"Tunafurahi kupata ushindi maana baada ya hapa tutaanza kubadilika. Timu imeanza kucheza vizuri sasa na baada ya mechi kadhaa tutaona mabadiliko zaidi," alisema.
Katika hatua nyingine, Rostand amemsifu straika wa Njombe Mji, Ditram Nchimbi kwamba alimpa changamoto kwa kupiga mashuti kadhaa langoni mwao kwani asingekuwa makini mambo yangekwend
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.