Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijiji ,unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu kimkoa kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco,utakao sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo havikupata huduma hiyo wakati wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili.
Akizungumza katika uzinduzi huo agosti 19 uliofanyika katika kijiji cha Luchelegwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi , Dkt . Medard Kalemani alisema kuwa, REA Awamu ya Tatu itatekelzwa kwa miaka mitano kuanzia sasa hadi kufikia 2021.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa,mara baada ya uzinduzi rasmi kimkoa kazi ya kusambaza umeme itaanza mara moja kwenye vijiji 173 kati ya 343 vilivyosalia awamu ya kwanza
“REA awamu ya Tatu imezinduliwa rasmi hapa kimkoa hapa kijiji Luchelegwa , mradi huu sasa utamaliza kazi ya kuunganisha huduma ya umeme katika vijijini vyote 343 vilivyoachwa katika Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi huo, ili kifikia idadi ya vijiji vyote 536 vya mkoa wa Lindi bara ifikapo mwaka 2021”, alisema Kalemani.
Dkt. Kalemani alisema kuwa REA Awamu ya Tatu itasambaza huduma ya umeme katika vijiji 120 wenye thamani ya zaidi bilioni 22 na awamu ya tatu vijiji 173 vitaungani umume wenye thamani ya shilingi bilioni 31 na vijiji 50 zitakuwa vya mwisho kumaliziwa
Dkt. Kalemani alitoa wito kwa wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya viwanda.
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Lindi Ramadhani Kaswa aliziomba taasisi za umma, dini, na mashirika mbalimbali kugharamia , kutandaza nyaya za umeme katika ofisi zao ili kuweza kuunganishwa na huduma ya umeme ambayo hupatikana kwa bei nafuu ya shilingi elfu 27 .
Kaswa aliwataka wananchi hao kulinda na kuitunza miundombinu ya mradi huo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla kwa kuwa miundombinu hiyo ni ya gharama kubwa.
Post a Comment