0
Rais Kim jong Un na Donald Trump Kulia
Image captionRais Kim jong Un na Donald Trump Kulia
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amesema kuwa hakuna tishio lolote la hivi karibuni kutoka Korea Kaskazini , licha ya Pyongyang kusema kuwa inapanga kushambulia eneo la Guam nchini Marekani.
Kuhusu Guam bwana Tillerson pia alimtetea rais Donald Trump ambaye ameitishia Korea Kaskzini kwamba ataikabili kivita.
Alisema kuwa rais Trump alitaka kutuma ujumbe kwa Korea Kaskazini.
Lakini rais huyo amejigamba katika mtandao wa Twitter kuhusu uwezo mkubwa wa zana za kinyuklia za Marekani.
Katika ujumbe wa mtandao wa Twitter uliochapishwa mwendo wa Alfajiri, rais Trump alisema kuwa silaha za kinyuklia za Marekani zimeimarika zaidi ya ilivyokuwa lakini akasema kuwa anatumai hatalazimishwa kuutumia uwezo huo.
Visiwa vya Guam nchini Marekani
Image captionVisiwa vya Guam nchini Marekani
Ujumbe huo wa Twitter unafuatia kuzuka mwa majibizano kati ya pande hizo mbili huku kisiwa hicho cha Guam ambacho ndio makao ya ndege za kivita za Marekani na watu 163,000 kikizungumziwa.
"Huku idara yetu ya maswala ya kigeni ikifanya kila juhudi ya kutatua swala hilo, kwa njia ya kidiplomasia ni lazima ifahamike kwamba jeshi la Marekani limeimarika na lina ulinzi mkali duniani''.
''Vitendo vya Korea Kaskazini vitashindwa na majeshi yetu itapoteza silaha na migogoro inayolenga kuanza'', aliongezea.

Post a Comment

 
Top