0
Rooney na wachezaji wenzake wa Everton baada ya kuisaidia timu hiyo kuilaza Gor Mahia ya KenyaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRooney na wachezaji wenzake wa Everton baada ya kuisaidia timu hiyo kuilaza Gor Mahia ya Kenya
Wayne Rooney ameiongoza klabu yake mpya Everton kuishinda klabu ya Kenya ya Gor kwa kufunga bao zuri katika mechi ya kirafiki iliodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa.
Mchezaji huyo alirudi katika klabu yake ya utotoni baada ya kuichezea Manchester united kwa takriban miaka 13.
Rooney aliiweka kifua mbele Everton kunako dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza ambacho Gor Mahia ilionekana kucheza vizuri kuwashinda wageni hao.
Hatahivyo Gor Mahia haikusubiri kwani baada ya mpira kuanzishwa katikati walipata kona iliopigwa na George Odhiambo ambapo ilimpata JacquesTuyisenge katika eneo zuri na hivyobasi kusawazisha kupitia kichwa kikali ambacho kipa wa Everton alishindwa kuokoa.
Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza timu hizo zilikuwa na sare ya 1-1.
Timu zote mbili zilifanya mabadiliko huku Rooney akitolewa baada ya kipindi cha kwanza
Bao la Rooney lilirudisha kumbukumbu za bao lake dhidi ya Arsenal akiichezea Everton.
Katika kipindi cha pili Everton ilionekana kuimarika zaidi huku ikitishia lango la Gor Mahia mara kwa mara.
Na ilipofika dakika ya 81 kipindi cha lala salama Everton ilijiweka kifua mbele kupitia kiungo wa kati Kieran Dowell aliyewageuza mabeki wa Gor Mahia na kucheka na wavu.

Post a Comment

 
Top