0

Leo July 13, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara ya Tsh 12.7 bilioni.

Washtakiwa hao waliachiwa huru mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis kuiomba Mahakama iwaachie chini ya kifungu cha 91(1) cha mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
Wengine walioachiwa huru mbali ya Masamaki wengine ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya, Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya, Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan.

Aidha, baada ya kesi hiyo kufutwa na washtakiwa hao kuachiwa huru, washtakiwa wenzao ambao ni Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Meneja wa Oparesheni za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis na Haroun Mpande wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT, TRA wamesomewa mashtaka mapya 110.

Katika mashtaka hayo ya uhujumu uchumi yamo ya kufuta data kwenye mfumo wa kompyuta, kughushi na kutakatisha fedha.

Post a Comment

 
Top