0
Liu Xiaobo amefariki
Image captionLiu Xiaobo amefariki
Mshindi pekee wa tuzo ya amani ya Nobel nchini China, Liu Xiaobo, amefariki.
Wakati wa kifo chake alikuwa na umri wa mika 61 na ni saa 48 tu zilizopita tangu alipoondolewa gerezani na kukimbizwa hospitalini, ili kutibiwa maradhi ya saratani.
Bwana Liu alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 11 jela, kwa kosa la kusambaza shinikizo kwenye mitandao, akitoa wito kwa China kukomesha utawala wa chama kimoja cha kisiasa.
Mataifa ya magharibi na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kote duniani, yamekuwa yakitoa wito kwa Beijing kumkubalia Bwana Liu Xiaobo kwenda nje ya nchi ili kutibiwa, lakini China ikakataa.
Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel China, marehemu Liu Xiaobo, aonekana akatika picha hii iliyopigwa siku mbili zilizopita akitoka Gerezani
Image captionMshindi wa tuzo ya amani ya Nobel China, marehemu Liu Xiaobo, aonekana akatika picha hii iliyopigwa siku mbili zilizopita akitoka Gerezani
Liu Xiaobo alikuwa mwaandishi na mwanasiasa, msomi mwenye sifa kubwa, ambaye daima alikuwa akishinikiza kuwepo kwa mabadiliko ya amani ya kisiasa.
Alikuwa mmojawepo wa mshirika mkuu wa wanaounga mkono kuwepo kwa maandamano ya demokrasia katika uwanja wa Tiananmen Square mnamo mwaka 1989.

Post a Comment

 
Top